Unordered List

Definition List

Lulu Michael Aaibiki, Hataki Kuchunguzwa Kwa Simu

Lulu
Kufikia sasa wafahamu kuwa kuna tetesi za Lulu Michael kunaswa live na polisi wakilana uroda yeye na Young D.

Mwigizaji wa filamu nchini Bongo Elizabeth Michael aka Lulu, amesema kuwa hatamani tena kutumia simu ya mkononi kwa kuwa anasumbuliwa mno na watu wasiokuwa na mambo ya msingi huku akitamani irudi enzi ya kutumiana barua.


Lulu aliyatamka haya baada ya mapaparazi kutaka kujua kama tukio ambalo linakisiwa kuwa la kweli kati yake na Young D lilifanyika.

Akiongea na paparazi ambaye aliweza kuipasha blogu yetu ya bkuHABARI, Lulu alisema kuwa kero hilo humfanya atamani kurudi katika enzi za kale za kuwasilia kwa kutumiana barua kwa njia ya posta.

“Nadhani sihitaji simu ya mkononi kwa sasa, mwenye shida na mimi atanitumia barua. Sijui, hata sijielewi nikasimame wapi, maana hata nikibadili nambari ya simu inasambaa kwa kasi sana,”alisema.

Lulu alibainisha kuwa kwa siku hupigiwa simu zisizokuwa na idadi na zisizo na faida kwake, lakini akakiri kwamba idadi kubwa ya watu wanaompigia simu ni mashabiki wake.


Cheki picha zilizotetemesha mtandao za Lulu alipopiga picha akiwa amevaa nyeupe na hairsyle mpya

“Ninapigiwa simu nyingi kwa siku ambazo ni kero kwangu, nafurahi sana ninapopigiwa simu na shabiki wangu, lakini wapo wanaopiga simu kutaka mambo ya ajabu.

Sawa ni wengi wao ni mashabiki wangu, lakini simu kwangu ni kero kubwa ingawa ni msaada mkubwa pia kwangu ni sehemu ya kitendea kazi.”
Lulu Michael Aaibiki, Hataki Kuchunguzwa Kwa Simu Lulu Michael Aaibiki, Hataki Kuchunguzwa Kwa Simu Reviewed by Admin on Sunday, December 15, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.