Unordered List

Definition List

Aunt Ezekiel Kubadili Dini, Ataka Kuwa Mlokole

Stori: Imelda Mtema
LICHA ya kubadili dini na kuwa muislam kisha kupewa jina la Rahma, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema sasa anatamani kurejea ‘ulokoleni’ na kumrudia Yesu kwa kuokoka.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, msanii huyo ambaye alibadili dini kutoka ukristo na kuwa muislam baada ya kuolewa na mumewe, Sunday Demonte alisema anajisikia kurudi kwenye ukristo kwa madai ya kumtumikia Mungu kikamilifu.

Akionesha msisitizo katika hilo, Aunt alisema moyo wake umekuwa ukitamani kusikiliza mafundisho na mahubiri ya kikristo pamoja na kusikiliza nyimbo mbalimbali za injili.

“Natamani sana kuokoka, mara nyingi nikisikia mahubiri au nyimbo za injili, moyo wangu hupata faraja kubwa sana,” alisema Aunt.

Wakizungumzia mawazo ya kuokoka ya msanii huyo, baadhi ya mashabiki wake walimshangaa huku wakionesha wasiwasi wake juu ya kusilimu na kudai huenda kubadili kwake dini ilikuwa danganya toto.

“Huyu si aseme tu uislam umemshinda? Kasilimu juzijuzi tu hapa na kudai ameanza kusali msikitini, leo anatuambia anatamani kuokoka, hawa mastaa wetu wanamchezea sana Mungu,” alisema Rahma wa Kinondoni jijini Dar.
GPL
Aunt Ezekiel Kubadili Dini, Ataka Kuwa Mlokole Aunt Ezekiel Kubadili Dini, Ataka Kuwa Mlokole Reviewed by Admin on Friday, December 27, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.