Sijui mambo mengine tuyaite ni upumbavu ama umbulala ama ushenzi...hapo utachagua wewe lakini imekuwa masikitiko makubwa watu kujiua ovyo kwa mambo ya kijinga.
Mwezi uliopita kulikuwa na habari ya kuchekesha na kuhuzunisha wakati uo huo baada wa shabiki wa Arsenal kulazimishwa kuangalia mkewe akiliwa uroda/ngono live mbele ya hadhira.
Sasa wakati huu mambo yamezidi kuharibika.
Jamaa ameamua kujimaliza uhai baada ya timu yake ya Manchester United kufungwa na New Castle.
Jamaa huyo(tumuite marehemu) kwa jina Jimmy Macharia(23) aliamua kwenda kujiunga na akina babu zake baada ya kujirusha kutoka orofa ya saba huko jijini Nairobi. Ukosefu Wa Akili.
Bila sababu za maana mtu anajitoa uhai kwa sababu ya mpira...Habari hii haitakuwa ya kwanza wala ya mwisho kwani blog hii pia ishawahi kuanika stori ya jombi flani aliyetaka usaidizi wa mamake baada ya kutiwa viboko vingi, kisa ni nini? Timu aliyokuwa akiishabikia imefungwa.
Kijana huyo aliyejitoa uhai (marehemu) labda alikuwa anategemewa na wazazi wake kwa mambo kadhaa kwa kuwa umri wake ni mdogo sana na anahitajika kujenga nchi.
Kulingana na habari za maofisaa ambao wanachunguza kisanga hicho, inadaiwa marehemu huyo aliamua kukatiza maisha yake baada ya kusema kuwa ameshindwa kustahimili kuangalia timu yake ikifungwa kimfululizo bila mpangilio.
Kweli huko ni kutumia akili?
Hakuna hata mchezaji mmoja anayekujua na wala hakuna wakati watakutambua.
Ni heri ujiue kwa sababu ya kushabikia timu yako ya nyumbani ambayo wawafahamu wachezaji wote na pia nirahisi wao kukutambua.
Wazo langu kwa wote wanaoshabikia mipira ya ugaibuni ni kuwa tabia za kufanyika kama mwaiabudu mipira muache. Kuna shughuli muhimu za kujenga taifa ambazo ni muhimu zaidi kuliko kukesha siku nzima kuangalia mipira ambayo haitakusaidia kamwe maishani mwako.
Ni masikitiko makubwa na pia ni aibu katika kizazi chetu cha kiafrika ambacho kinajali uhai wa binadamu na haakiruhusu watu kujiua ovyo bila sababu za maana. Alie na maskio na asikie
Chanzo cha habari ya tanzia ya shabiki huyo imetolewa kutoka gazeti la Standard

Shabiki Wa Manchester United Ajiua Baada Ya Kushindwa Kustahimili Kichapo Cha Mabao
Reviewed by Admin
on
Sunday, December 08, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano