Unordered List

Definition List

RAYUU ATAMANI KUCHUMBIWA NA KINGWENDU!!!

Rayuu
MSANII wa kike wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kwa kusema kuwa mwanaume sahihi kwake na anayestahili kumuoa ni Rashid Mizengwe ‘Kingwendu’ kwa kusema anaamini ndiye anaweza kuwa mwaminifu na kuishi naye kwa raha tofauti na mwanaume mwingine yoyote endapo atapata bahati ya kuolewa naye.


“Unapofika umri fulani suala la kuolewa si mjadala bali ni lazima iwe hivyo lakini shida inakuja je utaolewa na mwanaume anayekujali, kuheshimu na kukupenda? Basi kwangu nataka kuolewa na mwanaume kama Kingwendu naamini nitakuwa na amani raha mstarehe, tofauti na kama nitapata sharobaro sina hakika kama atanijali,”anasema Rayuu kwa fulaha.


kingwendu_Rashid_Mwinsheshe
Rayuu alisema hayo alipoongea na Maskani Bongo katika mahojiano yake na gazeti la GPL kuhusu mume gani bora kwake na angependa kuolewa naye na kuishi kama mke na mume, msanii alisema kuwa anahitaji mtu aliyetulia sambamba na umri wa makamo na mtu anayempenda sana kama awe mumewe ni msanii mwenzake Kingwendu au anayefanana naye.
RAYUU ATAMANI KUCHUMBIWA NA KINGWENDU!!! RAYUU ATAMANI KUCHUMBIWA NA KINGWENDU!!! Reviewed by Admin on Friday, December 20, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.