Unordered List

Definition List

SNURA: Wema Sepetu Amenitoa Kwa Mziki

Snura
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ‘Mama Majanga’ ametoa ya moyoni na kumshukuru aliyekuwa rafiki yake wa damu, Wema Sepetu kwa kuwa ndiye aliyembunia vazi la muziki na fedha ya kurekodi wimbo wake wa kwanza.

Akistorisha na paparazi aliyeiarifu bkuHABARI, Snura alisema fedha ya Wema ilihusika kumtoa kimuziki kwani wakati akirekodi wimbo wake wa kwanza, sauti yake iliingia kwenye wimbo huo na vazi lake la shoo ya kwanza alilibuni Wema ambapo mpaka sasa analiendeleza, hivyo anamshukuru sana na anamuombea kwa Mungu ambariki zaidi.
Wema Sepetu


“Namshukuru Wema, kwani alihusika sana kwenye wimbo wangu wa kwanza wa ‘Shogaake Mama’ kwani fedha yake ndiyo ilitumika kurekodi wimbo huo pia aliingiza sauti yake kwenye wimbo huo, alinibunia vazi la shoo yangu ya kwanza ambalo ninaliendeleza mpaka sasa,” alisema Snura.
SNURA: Wema Sepetu Amenitoa Kwa Mziki SNURA: Wema Sepetu Amenitoa Kwa Mziki Reviewed by Admin on Monday, December 30, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.