Unordered List

Definition List

Belle 9 Kutoa Hit Song Na Wyre!!!

Belle 9 na Kevin Wyre.
Hitmaker wa Masogange, Belle 9 amesema baada ya kufunga mwaka na wimbo wa ‘Wanitaka’ kinachofuata ni kolabo na msanii wa Kenya Wyre ili kufungua mwaka 2014.

Akizungumza na bongo5, Belle amesema muziki wa sasa unabadilika hali iliyomfanya afikirie kuongeza nguvu kwa kumshirikisha Wyre.
“Nimekuwa nafanya muziki wangu kiubunifu sana. Ukiangalia nyimbo zangu zote zipo tofauti tofauti sana,ukianzia na wimbo wa Masogange,Nilipe Nisepe na Listen, zina utofauti sana. Hali hii inatoka na kuangalia Watanzania wanataka nini ndio maana hata sasa hivi nimeamua kufanya wimbo na Wyre wa Kenya na producer atakuwa Sappy yule aliyofanya wimbo wa Prezzo ‘Celebration of Life’, Alisema Belle.
Sappy ni producer wa Tanzania anayefanya kazi kwenye studio za Homeboyz Production na ndiye aliyetengeneza hit ya Redsan, Badder Than Most. credit-bongo5
Belle 9 Kutoa Hit Song Na Wyre!!! Belle 9 Kutoa Hit Song Na Wyre!!! Reviewed by Admin on Friday, December 20, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.