Unordered List

Definition List

Tabia Ya Lulu Kupima UKIMWI Kila Wakati...Kunani?!?

Lulu Michael

KAULI aliyoitoa msanii nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhusu kupima mara kwa mara maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, imeibua utata mkubwa miongoni mwa wadau wakihoji ana nini moyoni mwake?

Katika tamasha maalum la Siku ya Ukimwi Duniani lililofanyika Desemba Mosi, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, Lulu akiwa miongoni mwa waliohudhuria, alikiri kupima virusi vya ugonjwa huo mara kwa mara na kuwataka vijana wengine waige mfano wake.

“Vijana wengi waoga kujitokeza kupima Ukimwi, wanadhani kwa kufanya hivyo ni kujitafutia hofu ya kifo kitu ambacho si kweli.

“Hata mimi nilikuwa mwoga sana lakini baada ya kupata elimu stahiki juu ya umuhimu wa kujua afya kila mara, nimekuwa nikipima mara kwa mara, hivyo hata ninyi nawaasa mjenge tabia ya kupima UKIMWI mara kwa mara,” alisema Lulu.

Baadhi ya wadau walihoji kulikoni msanii huyo mwenye historia mbaya huko nyuma, hasa ya starehe awe na tabia hiyo ya kupima Ukimwi mara kwa mara?


Wengi walihoji je amekuwa akipima mara kwa mara kwa sababu huwa anabadilisha wanaume mara kwa mara? Wengine walihoji amekuwa hatumii kinga?

“Kwa nini amekuwa na tabia ya kupima UKIMWI mara kwa mara? Ina maana huwa hatumii kinga? Au ni uaminifu mdogo katika uhusiano?” alihoji mdau mmoja ambaye pia ni msanii mkubwa wa filamu za Kibongo akiomba kusitiriwa jina.

Hivi karibuni dada huyu aliweza kukataa katakata kuchumbiwa na staa Diamond Platinumz, ama Lulu ana wachumba wengine wa kando ambao bado hawajawaweka hadharani.
Tabia Ya Lulu Kupima UKIMWI Kila Wakati...Kunani?!? Tabia Ya Lulu Kupima UKIMWI Kila Wakati...Kunani?!? Reviewed by Admin on Thursday, December 05, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.