Unordered List

Definition List

Venessa Mdee: Uoga Ulinifanya Nisionyeshe Kipaji Changu

Akiongea na Bongo5 leo, Vanessa amesema muziki anaoufanya sasa hivi ni muziki aliokuwa nao miaka 4 iliyopita lakini alishindwa kuonyesha kipaji chake kutokana na kuogopa.

“Kitu ambacho kimechelewesha kuonyesha kipaji changu, I think kila kitu ni timing. Na kitu kingine ambacho nilikuwa na tatizo nacho nilikuwa sina ile confidence ya kupanda stejini, nilikuwa narekodi muziki kwa muda mefu sana, muziki ambao niko nao ni wa miaka mitatu minne lakini nilikuwa sina ile conficance ya kuitoa because in my head is was imperfect. Mimi ni mtu ambaye nataka niwe perfect,” amesema Vanessa.

“Lakini kuna mtu alinikalisha akaniambia ‘sikiliza dada muziki wako hata siku moja kwenye sikio lako hautausikia kama ni mzuri hundred % siku zote, siku zote utakuwa unajitolea kasoro, unatakiwa ukifikia asilimia 75 iachie kwa sababu that’s good enough’. Mimi nikachukua huoushauri nikawa naufanyia kazi kadri siku zinapozidi kwenda japo bado sijafikia sehemu ambayo yaani nipo confident kabisa, lakini kiasi chake nimeanza kujaribu kujiachia.

”Katika hatua nyingine Vannesa ambaye atafanya show katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 jijini Mwanza ameweka wazi mipango yake ya kuachia album.“Nimekuwa kwenye mipango ya kufanya collabo na wasanii mbalimbali wa Afrika ingawa nisingependa kuliweka wazi zaidi, lakini nyimbo zinakuja na nyingine zinaweza zikaja pamoja kwenye album yangu,” amesema Vee.

“Album yangu ipo naifanyia kazi lakini haitatoka mpaka mwakani. Itakuwa inaitwa ‘Money Monday’. Mimi ninapenda sana kutengeneza album ili mashabiki wangu wapate taste ya muziki wangu na nina muziki mwingi ambao umekaa studio sasa kwa nini nisitengeneze album nikaiachia tu? Japo watu wanasema soko letu limekuwa gumu na kuna watu wanaiba muziki, mimi nimeona kuna platform mbalimbali kama Mkito. Mimi naweza nikatumia iTunes hata watu ambao wapo nje ya nchi wanaweza kupatana kusikiliza muziki wa kitanzania kutokana na platform ambazo mimi nimeweka.”
Venessa Mdee: Uoga Ulinifanya Nisionyeshe Kipaji Changu Venessa Mdee: Uoga Ulinifanya Nisionyeshe Kipaji Changu Reviewed by Admin on Saturday, August 09, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.