Unordered List

Definition List

Diamond Platnumz Apigwa Msasa Na Kikosi Cha Kuzuia Dawa Za Kulevya

Stori: Shakoor Jongo na Makongoro Oging’

Ni kweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguuyao kumfuatilia, Amani limesheheni.

Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.

Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambayehakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.

MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.“ Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.

Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar.
GPL
Diamond Platnumz Apigwa Msasa Na Kikosi Cha Kuzuia Dawa Za Kulevya Diamond Platnumz Apigwa Msasa Na Kikosi Cha Kuzuia Dawa Za Kulevya Reviewed by Admin on Thursday, August 21, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.