Unordered List

Definition List

Ommy Dimpoz Awachanganya Jokate Na Venessa Mdee

Acha kabisa! Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa wenzake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money,
Ijumaa Wikienda limeinyaka.

Kikizungumza na gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa Bongo (Ijumaa Wikienda), chanzo makini kilisema Jokate na Vanesa kwa sasa ni kama chui na paka kufuatia hivi karibuni Jokate kudaiwa kuingilia penzi la mwanzake na mpaka sasa eti ndiye aliyeshikilia usukani. “Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja. “Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizi, mwanahabari wetu alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Ehee! Ndiyo nasikia kwako, kwani wasanii haturuhusiwi kupendana jamani, hata Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) alisema tuwe pamoja kwa hiyo Jokate ni rafiki yangu wa karibu na huyo Vanessa sijawahi kuwa na uhusiano naye but (lakini) alikuwa mshikaji tu.”

Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa ziligonga mwamba baadaya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.

Juzikati picha za Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali haliiliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.
Ommy Dimpoz Awachanganya Jokate Na Venessa Mdee Ommy Dimpoz Awachanganya Jokate Na Venessa Mdee Reviewed by Admin on Tuesday, August 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.