Unordered List

Definition List

Lady Jaydee Na Mumewe Wameachana!? Jide Aishi Hoteli Pekeyake

Stori: Global Publishers

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika, anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu.

Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005.

Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake. Hata hivyo, gazeti dada ya hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita lilizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli.

Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani. Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona Gardner miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao!

Juzi, mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba kutokana na kuwa mteja wa muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa chumba chake anaondoka nayo.

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide (jina tunalo) alithibitisha msanii huyo kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa hiyo, kwa kile alichodai kuwa haieleweki. “Ni kweli Anaconda (Jide) anaishi pale, wewe nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au hayupo,” alisema mtu huyo.

Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendeleahuku ikielezwa kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye anayepatika kirahisi katika simu yake ya mkononi.
Lady Jaydee Na Mumewe Wameachana!? Jide Aishi Hoteli Pekeyake Lady Jaydee Na Mumewe Wameachana!? Jide Aishi Hoteli Pekeyake Reviewed by Admin on Thursday, August 21, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.