Unordered List

Definition List

SABBY WA BONGO MUVI: RUSHWA YA NGONO BONGO MUVI IMENITESA

Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa akifurukuta kutoka kisanii.

Akizungumza na Ijumaa Sabby alisema, tatizo hilola rushwa anaweza kuwa miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna baadhi walipokuwa wakitolewa nje, walikuwa wanajenga bifu naye na wengine kumtishia kumharibia.

“Mimi kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka leo ni jinsi wanawake tunavyodhalilishwa kila siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi mpaka nafikia hapa leo, ila namshukuru Mungu siku zote,” alisema Sabby ambaye ameng’ara kwenye filamu kama vile Siri ya Gining, Hard Price, Moto wa Radi,Dr. Ray na nyinginezo.
SABBY WA BONGO MUVI: RUSHWA YA NGONO BONGO MUVI IMENITESA SABBY WA BONGO MUVI: RUSHWA YA NGONO BONGO MUVI IMENITESA Reviewed by Admin on Friday, August 29, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.