Unordered List

Definition List

Aunty Lulu: Sina Kinyongo Na Mapenzi Ya Wastara Na Bond

Stori: Gladness Mallya

BAADA ya kuachwa na mpenzi wake wa siku nyingi Bond, ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa filamu, Wastara Juma, Aunty Lulu amekubali yaishe na sasa hana tena kinyongo nao.

“Mimi sina tena kinyongo na Wastara, vile nilikuwa namfanyia tu vituko, lakini kwa sasa asiniogope wala asiwe na wasiwasi na mimi, nimeshaachana na Bond japokuwa tulitoka mbali sana na hakuna wanamke anayemjua kama mimi, siku ya harusi yao nitacheza mpaka asubuhi,”alisema Aunty Lulu.

Msichana huyo aliyepata umaarufu baada ya kutwaa taji la Kimwana Twanga Pepeta, alitoa kauli hiyo hivi karibuni maeneo ya Kinondoni baada ya kutakiwa kutoa tamko juu ya uhusiano wa wawili hao, ambaoawali alikuwa akiwatupia madongo na kuwapiga vijembe.Alisema kwa sasa hana kinyongo na Wastara na amebariki uhusiano wao wa kimapenzi.
Aunty Lulu: Sina Kinyongo Na Mapenzi Ya Wastara Na Bond Aunty Lulu: Sina Kinyongo Na Mapenzi Ya Wastara Na Bond Reviewed by Admin on Thursday, August 21, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.