Unordered List

Definition List

Mchekeshaji Kingwendu Na Stori Ya Mkewe Kubakwa, Ana Yapi?

Muigizaji wa filamu za Kiswahili,mchekeshaji Kingwendu yuko katika wakati mgumu baada ya mkewe kubakwa na jirani yake wakati akiwa amelewa pombe.

Muigizaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa alizipata habari hizo wakati ambapo yuko safarini na majirani walimueleza kilichotokea kuwa mkewe na jirani huyo aliyembaka mida ya saa tano usiku wote walikuwa wamelewa.

”Kama ulivyosikia hiyo habari, mimi nilikuwa sipo ndo nimerudi hivi, nataka nianze kufuatilia sheria sema sasa hivi nimefiwa na dada yangu tunapeleka msiba kijijini na baada ya hapo ninapumzika kesho tu halafu ninasafiri Nairobi, nikirudi Nairobi tarehe tano kuanzia tarehe sita ndo naanza kufuatilia.” amesema Kingwendu.

Mchekeshaji huyo ameumizwa na kitendo hicho na ameamua kufuata taratibu za kisheria ili haki itendeke. “Kutokana na kitendo alichokifanya na mimi nimejisikia vibaya, inanibidi nimtafute huyu bwana nimpate ili nimpeleke mahakamani, mkewangu bado niko naye, sema huyu jamaa aliyefanya unyamaa huu yupo jirani. Mke wangu alikuwa amelewa na jamaa naye alikuwa amelewa. Mke wangu sijui alikuwa anatoka wapi saa tano usiku ndo akakutana na huyo jamaa, majirani ndio walivyoniambia hivyo, walinipigia simu wakati nipo Shinyanga huko.” Source: Bongo5
Mchekeshaji Kingwendu Na Stori Ya Mkewe Kubakwa, Ana Yapi? Mchekeshaji Kingwendu Na Stori Ya Mkewe Kubakwa, Ana Yapi? Reviewed by Unknown on Friday, August 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.