Unordered List

Definition List

Mrisho Mpoto Nusra Afanyiziwe Na Majambazi Waliokuwa Wakimnyemelea

Msanii wa mashairi na mwimbaji Mrisho Mpoto jana amenusurika kuibiwa mamilioni ya hela alizokuwa akienda kununua nyumba huko Kigambani...


Mchezo mzima ulianzia Mbagala alipoenda kutoa hela kwenye Bank fulani ili aende kununua nyumba alipomaliza kuchukua hela alipanda gari yake akiwa njiani gari moja lilikuwa likimfuata nyuma na jingine lilikuwa mbele yake na lilikuwa likimzuia asipite, kiufupi alikuwa amewekwa 'mtukati' wakisubiri wafike sehemu nzuri wamfanyizie.

Kwa bahati nzuri mchezo huo wa majambazi ulishtukiwa na bank na kumpigia simu Mpoto kumtaarifu kuwa aelekee kituo cha polisi cha karibu , ambapo pia polisi walimpigia simu na kuja kumsaidia ndio jamaa (majambazi) waliposhtukia na kutokomea kusiko julikana......
Mrisho Mpoto Nusra Afanyiziwe Na Majambazi Waliokuwa Wakimnyemelea Mrisho Mpoto Nusra Afanyiziwe Na Majambazi Waliokuwa Wakimnyemelea Reviewed by Unknown on Saturday, August 02, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.