Unordered List

Definition List

Diamond Platnumz asikitishwa na kitendo hiki alichofanyiwa nchini Ujerumani…

Kama msanii ni furaha kwako kuona unapoalikwa kwenda kupiga show nchi za wenzetu unapata muda wa kutosha kukaa na mashabiki wako sababu ni nadra sana show kama hizi zitatokea.

Jana Diamond alikua anapiga show kubwa nchini ujerumani na kuashiria kwamba ilikua kubwa angalia jinsi huu ukumbi ulivyokua mkubwa.

Kilichomsikitisha Diamond ni kitendo cha promota wake kumpeleka kwenye shoo hii mida ya alfajiri huku akiwachosha mashabiki wake waliotoa mkwanja kuja kumuangalia.

Diamond alisema haya kuhusiana na hii ishu ”kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamuakujitolea kuja kwa wingi kutusupport vijana wao, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia na kuwadisappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi….”



Chanzo: Vibe
Diamond Platnumz asikitishwa na kitendo hiki alichofanyiwa nchini Ujerumani… Diamond Platnumz asikitishwa na kitendo hiki alichofanyiwa nchini Ujerumani… Reviewed by Admin on Sunday, August 31, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.