Unordered List

Definition List

Tisha!!! Uganda Yalegeza Kamba Kuhusu Sheria Kali Za Ushoga

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.


Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika kuingilia kati.
Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Ugandahasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.
Tisha!!! Uganda Yalegeza Kamba Kuhusu Sheria Kali Za Ushoga Tisha!!! Uganda Yalegeza Kamba Kuhusu Sheria Kali Za Ushoga Reviewed by Unknown on Saturday, August 02, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.