Unordered List

Definition List

Diamond Platnumz Ajibu Hutma Za Kumtumia Wema Sepetu Kimapenzi

Baada ya mashabiki wa mwanadada Wema "kumjia juu mwanamuziki Diamond Platnumz" kuhusu tuhuma za yeye kumtumia mwanadada huyu kimwili zaidi bila kumuendeleza, hatimaye raisi huyu wa kundi la WCB ameamua nayeye kufunguka haya mazito juu ya kauli hizo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao ule maarufu wa kijamii Diamond ameandika haya..

“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...

Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!

Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!"Diamond
Diamond Platnumz Ajibu Hutma Za Kumtumia Wema Sepetu Kimapenzi Diamond Platnumz Ajibu Hutma Za Kumtumia Wema Sepetu Kimapenzi Reviewed by Admin on Friday, August 15, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.