Unordered List

Definition List

Tundaman Matatani Kenya, Baada Ya Picha Ya Kimahaba Na Nyota Ndogo, Sasa Ni Polisi

Tundaman wiki hii amekuwa akimake headlines kwa mitandao ya kijamii nchini Kenya na Tanzania pasipo na ajenda yeyote ya maana.

Aliweza kupiga picha na mpenzi wake wa kando msanii maarufu Mombasani Nyota Ndogo...



...na sasa ameingia katika rada ya polisi wa trafiki nchini Kenya baada ya kunaswa na polisi kwa kosa la kuendesha gari lake kwa kasi pamoja na kuchezesha nyimbo kwa sauti ya juu.


Baadaye iligundulika kuwa Tundaman alikuwa anafanya haya yote ili kupata umaarufu pamoja na atenshen kutoka kwa hadhira yake na kesi ya kushikwa na polisi ilikuwa ni njama tu ya uongo.

Lakini hii haijamshawishi Kisauni DCIO, Joseph Kioko, ambaye ameapa kuwa Tundaman atashtakiwa kama atapatikana na kosa la kutumia kikosi cha polisi kujiongezea umaarufu.
Tundaman Matatani Kenya, Baada Ya Picha Ya Kimahaba Na Nyota Ndogo, Sasa Ni Polisi Tundaman Matatani Kenya, Baada Ya Picha Ya Kimahaba Na Nyota Ndogo, Sasa Ni Polisi Reviewed by Admin on Wednesday, August 20, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.