Unordered List

Definition List

Mch. Gwajima Anunua Helicopter Ya Kwanza Kabisa Ya Kusambaza Injili

Habari ambazo zimethibitishwa na facebook page ya kanisa la Ufufuo na Uzima zinasema kuwa Helcopta hiyo imewasili nchini tayari na sasa inafanyiwa assembling kwa ajili ya kuanza kuruka jumatatu hii.

Tukio ambalo limelifanya kanisa hilo kuandaa ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kupokea helcopta hiyo itakayotumika kusambaza injili Tanzania.

Helcopta hiyo aina ya R44 ni mali ya kanisa la Glory of Christ T Church ambalo liko chini ya mch. Gwajima.

Akiongea Jumapili iliyopita kanisani kwake Kawe Mch. Gwajima alisema huku akimsimamisha Mjapani mmoja ambaye kwa mujibu wa Mch huyo ndiye aliyefanikisha ununuzi wa chopper hiyo ya kwanza nchini kutumika katika kusambaza injili.

Aidha, Mchungaji Gwajima alitumia muda huo kutoa Ufafanuzi juu ya kuwepo kwa taarifa za yeye kushirikiana na Nabii maarufu GeorDavie kuzindua helcopta hiyo alisema,"Nabii GeorDavie amepanga kukodi helcopta aina sawa na yetu (R44) na atatua nayo kwenye kanisa lake (ambalo pia lipo maeneo ya Tanganyika Packers) akitokea Arusha. lakini mjue wote kuwa helcopta hiyo si ambayo kanisa la Ufufuo na Uzima imeinunua bali imekodiwa seacliff na wala hatujaandaa mkutano wa pamoja na Nabii huyo" mwisho wa kunukuu.

Hii inakuwa Helcopta ya kwanza kutumika kuhubiri injili ikiwa ni mali ya kanisa. Ibada ya shukrani kanisani Ufufuo na Uzima itahudhuriwa na waimbaji kama Munishi aliyekwisha wasili na Malebo (ameokoka), Rose Muhando, Bony mwaitege, John Lisu, Upendo Nkone, Flora Mbasha, Christina Shusho na wengine wengi..
Mch. Gwajima Anunua Helicopter Ya Kwanza Kabisa Ya Kusambaza Injili Mch. Gwajima Anunua Helicopter Ya Kwanza Kabisa Ya Kusambaza Injili Reviewed by Admin on Tuesday, August 05, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.