Unordered List

Definition List

Wema Sepetu Ajutia Kwa Nini Amerudiana Kimapenzi Na Diamond Platnumz

Takribani wiki sasa kumekuwana taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko sawa katika mahusiano yake ya kimapenzi na nguli wa Bongo Fleva, Diamond Plutnumz….

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na Wema, imefika mahali Wema anajuta kuwa na Diamond kwa sababu ya kuandikwa kwa mambo mengi yasiyo na ukweli na yanayomfedhehesha moyoni….

Rafiki huyo amedai kuwa mara kwa mara Wema amekuwa akijiuliza sababu ya kuandikwa taarifa mbalimbali zisizo na kichwa wala miguu ambapo mwisho wa yote hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa na mahusiano na Diamond….

“Wakati mwingine anasema angelijua bora angebaki bachela kwani kuna kikundi cha watu hakipendi kumuona akiwa na Diamond hivyo kinafanya kazi ya kumzushia taarifa zisizoeleweka kila mara kwa lengo la kumshushia hadhi,” kimesema chanzo hicho.

Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho ni kwa kiasi gani Wema anamwamini Diamond kilisema:“Ukweli ni kwamba Wema anampenda sana Diamond lakini hamwamini kwa sababu wakati mwingine taarifa zinazoandikwa magazeti hutolewa na Diamond mwenyewe, hali hiyo inampa wakati mgumu sana Wema kujua ashike wapi na wapi apaache,”

“Unajua Diamond haaminiki, unaweza kukuta Wema anagombana na watu kumbe mtoa taarifa ni Diamond mwenyewe.”
Wema Sepetu Ajutia Kwa Nini Amerudiana Kimapenzi Na Diamond Platnumz Wema Sepetu Ajutia Kwa Nini Amerudiana Kimapenzi Na Diamond Platnumz Reviewed by Admin on Wednesday, August 13, 2014 Rating: 5

1 comment:

  1. tulia wema mchimba kisima huingia mwenyewe

    ReplyDelete

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.