Unordered List

Definition List

Aunt Ezekiel Amchafukia Diva Kuhusu Uzushi Wa Ujauzito

JAMBO limezua jambo! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi ‘Diva’ kwa madai kwamba amemtangaza mitandaoni kuwa amepachikwa ujauzito na mume wa mtu ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Peter ‘Moze Iyobo’, jambo ambalo ni uongo.

Akizungumza kwa masikitiko ya hali ya juu, Aunt alisema kuwa hakutegemea mtu kama Diva angetumia nafasi yake ya utangazaji kumchafua akimsingizia kuwa ni mjamzito, jambo ambalo limemsababishia matatizo kwenye ndoa yake na mumewe Sunday Demonte.

“Mwanamke kuwa mjamzito si jambo baya lakini kunichafua mbele ya jamii eti nina mimba ya Moze Iyobo, imeniumasana.“ Hebu vuta picha wakwe, mawifi na mashemeji ambao tayari wameshasikia na kusomakwenye ukurasa wa Diva, akisema mimi nina mimba ya yule mtoto, dah! Nimeumia sana, kwa kweli siwezi kuliacha lipite hivihivi. “Huyo Diva lazima nitasimama naye mahakamani,” alisema Aunt.

Hivi karibuni, kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diva aliandika: “Wakati sakata la mtoto mzuri Aunt Ezekiel ana mimba ya Moze Iyobo likipamba moto, mimba ambayo ni tangu Mwezi wa Ramadhan, sasa hesabuni miezi, hapa ni miezi miwili au mitatu.
Aunt Ezekiel Amchafukia Diva Kuhusu Uzushi Wa Ujauzito Aunt Ezekiel Amchafukia Diva Kuhusu Uzushi Wa Ujauzito Reviewed by Admin on Saturday, August 30, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.