Unordered List

Definition List

Wema Sepetu Adai Hataki Laana Za Mamake Mzazi

NYOTA wa Filamu za kibongo Wema Sepetu amesema kuwa katika maisha yake anajitahidi hakosani na mama yake mzazi, Miriam Sepetu ili kukwepa kupata laana ya kile ambacho anaweza kumtamkia na kuharibu mwelekeo mzima wa malengo yake aliyojipangia kuyatimiza akiwa ndani ya ndoa yake……

Akizungumza na Mpekuzi, Wema alisema kuwa ndio maana kipindi ambacho mama yake hakutaka kuolewa na mchumba wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ hakupenda kutumia nguvu ama uwezo wake wa kifedha kumpuuza mzazi wake kwani anaamini angemuumiza na kumfanya amtamkie maneno mabaya.

“Natambua fika kuwa Mungu ametuagiza kuwaheshimu wazazi wetu kwani hawa ni miungu wadogo, wakitamka neno lolote baya baada ya kuwaudhi huwa linaumbika na kuwa shida kwa mhusika, ndio maana wakati anaweka mikingamo ya mimi kuolewa na Diamond sikulazimisha bali niliendelea kumsihi akubali.” Alisema Wema.

Penzi la Wema na Diamond linazidi kupamba moto hasa baada ya hivi karibuni kuvishana pete nyingine ya uchumba baada ya mama Wema kubariki penzi lao
Wema Sepetu Adai Hataki Laana Za Mamake Mzazi Wema Sepetu Adai Hataki Laana Za Mamake Mzazi Reviewed by Unknown on Thursday, August 07, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.