Unordered List

Definition List

DJ G-Lover Atofautisha Kati Ya Diamond Na Alikiba Kimziki

Moja ya mdau mkubwa wa muziki nchini na mmiliki wa G Records, studio iliyomtoa Alikiba, Guru Ramadhan aka DJ G-Lover, amezungumzia tofauti iliyopo kati ya Diamond na Alikiba aliyewahi kuwa chini yake.


Akizungumza na Vijimambo, Lover ambaye akiwa meneja wa Alikiba walitoa album mbili, amewaka bayana uwezo wa kila msanii na jinsi walivyojikuta kwenye biashara.

“Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi,” amesema G.

“Lakini unapokuja kibiashara Diamond huwa anazungumza kuwa yeye muziki wake anaufanya kibiashara na ndo maana ana team work kubwa ambayo inamsaidia yeye kujua ni kitu gani anatakiwa kufanya, kuna kitu gani anatakiwa kukifanya kwa upande wa muziki.
Sasa kwa upande wa Ali kwa sasa hivi, kwa kipindi niko naye nilikuwa na team ambayo hata yeye alikuwa hajui mimi nipo na akina nani nyuma yangu. Alikuwa anajua kuwa yupo G, lakini nyuma yangu nilikuwa na watu takriban thelathini ambao ni team work ambayo ilikuwa inafanya kazi kwa Ali Kiba kujuani kitu gani na kitu gani tunatakiwa tufanye ili afike na mpaka akafika hapo,” aliongeza.

“Diamond naye anafanya vitu kama hivyo, unaweza kuona Diamond ana team ya watu watatu tu au wanNe ambao wanamsaidia, kwaHiyo utaona Diamond kuna watu kibao ambao amewapa ajira. Kwa hiyo Diamond hawezi kuwaangusha watu ambao wapo nyuma yake ambao wamepata ajira kutoka kwake. Kwa mfano kuna utofauti mkubwa ambao Diamond amekuja nao ambao ukiangalia ni utaratibu uleule ambao nilikuwa nikiufanya kwa Ali. Kwa hiyo sijui kuna utofauti gani kati ya management ya Diamond na ya Ali Kiba ya sasa hivi."
DJ G-Lover Atofautisha Kati Ya Diamond Na Alikiba Kimziki DJ G-Lover Atofautisha Kati Ya Diamond Na Alikiba Kimziki Reviewed by Admin on Sunday, August 03, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.