Unordered List

Definition List

Wastara Anunua Chombo Kimpya

CHEREKO! Ikiwa umepita mwaka mmoja tangu mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ afariki dunia, msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma ameongeza ndinga mpya na kuiacha ile ya zamani kwa muda.

Akizungumza na paparazi wetu, Wastara alisema gari hilo aina ya Toyota Cami alinunua kwa shilingi milioni kumi na tano za kibongo na anamshukuru Mungu kwani fedha hizo zimetokana na muvi zake hivyo kwa sasa anamiliki magari mawili.

“Namshukuru Mungu kwakuendelea kunipigania kwani mafanikio haya siyo kwa nguvu zangu bali ni kwa neema yake tu, ukweli kazi ya filamu inalipa ndiyo maana naipenda kwani gari hili limetokana na filamu zangu nilizocheza,” alisema Wastara.
Wastara Anunua Chombo Kimpya Wastara Anunua Chombo Kimpya Reviewed by Admin on Monday, August 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.