Unordered List

Definition List

Wajua Sababu Kuu Ya Dogo Janja Kuacha Shule!?

Rapper kutoka Arusha, Dogo Janja ameamua kuacha shule ilikusomea masomo ya muziki.

Akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, Janjaro amedai kuwa usumbufu aliokuwa akiupata shuleni ndio sababu kubwa iliyomfanya aache shule.

“Shule ambayo mimi nimesoma nilikuwa napata matatizo kwa sababu kitu kidogo ambacho mnaweza mkafanya wote lakini wewe ukaonekana chanzo. ‘Msanii mhuni, huyu hivi,” alisema rapper huyo.

“Sometimes unaweza ukawa unasoma watu wengi wako dirishani wanapita wanakuangalia. Au unaweza ukakosea.. yaani wanakuwa wewe ni mtu ambaye upo sahihi all the time. Kwa mfano labda unajua zile za kushtukizwa ‘fulani jibu swali’ kila saa unaulizwa wewe,” aliongeza. “Kwa hiyo unakuwa hakuna pale Uabdul, unakuwa unaweka Ujanjaro Udogojanja. Kwa sababu unajua ile kushtukizwa kila saa unakuwa unahisi kama mwalimu anakuandama sana. Au kwenye mtihani, mnaweza mkawa mnafanya wote mtihani lakini mwalimu anakuja kukusimamia wewe, anakukazia kinoma."
Wajua Sababu Kuu Ya Dogo Janja Kuacha Shule!? Wajua Sababu Kuu Ya Dogo Janja Kuacha Shule!? Reviewed by Admin on Wednesday, August 13, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.