Unordered List

Definition List

Penny Afunguka: Nina Uhusiano Na Sitaki Kuskia Stori Za Diamond Platinumz

ZILIPENDWA wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’,  amefunguka kuwa hataki kumsikia mpenzi wake huyo wa zamani kwa madai kuwa amefungua ukurasa mpya wa uhusiano na mtu ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumweka wazi.

Penny
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini Dar wakati akizungumza na gazeti hili lililotaka kujua anazungumziaje tuzo saba za Kilimanjaro alizojizolea Diamond ambapo  majibu yaliyopatikana yalikuwa: “Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu zake, mimi sitaki.”

Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani alisema: “Mnamjua” na kuicha historia ikibaki kuwa Penny na msanii huyo waliwahi kuwa katika mapenzi mazito ya njiwa kabla ya kumwagana na mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu, ambaye mwenyewe anapenda aitwe mke mtarajiwa. Hahahaha!

Diamond Platinumz
Penny Afunguka: Nina Uhusiano Na Sitaki Kuskia Stori Za Diamond Platinumz Penny Afunguka: Nina Uhusiano Na Sitaki Kuskia Stori Za Diamond Platinumz Reviewed by Admin on Wednesday, May 14, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.