Unordered List

Definition List

Aunty Lulu Avua Nguo Hadharani Baada Ya Pombe Kumzidi Kichwa

Msichana wa mjini asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’, kwa mara nyingine amefanya kituko cha aina yake baada ya kuzua timbwili kisha kusaula nguo zote hadharani bila kujali yupo ukweni.

Aunty Lulu ana uhusiano wa kimapenzi na kijana anayejulikana kwa jina moja la Amani.

Habari zisizokuwa na chembe ya ‘dauti’ zilidai kuwa hivi karibuni, Aunty Lulu na Amani walikuwa wakipata kinywaji kwenye baa moja iliyopo jirani na nyumbani kwa wakwe zake maeneo ya Majohe, Dar ndipo ukaibuka ugomvi kati yao na kusababisha pachimbike.

Chanzo hicho kutoka ndani ya familia ya wakwe zake Aunty Lulu, kilidai kwamba mwanadada huyo alizua timbwili alipokuwa akipigana na Amani.

Ilisemekana kwamba katika hali ya kushangaza, Aunty Lulu alikwenda mbali zaidi alipovua nguo hadharani na kubaki mtupu hivyo kuwalazimu watu wenye busara kumshika na kumsihi avae nguo kisha walimpeleka nyumbani wanakoishi maeneo hayohayo ya jirani na wakwe zake.

“Yaani Aunty Lulu anamng’ang’ania kwa nguvu ndugu yetu Amani wakati familia nzima haimtaki kwa sababu ya tabia zake hizo, hii ni mara ya pili kuvua nguo hadharani.

“Ukweli hata baba mkwe hataki kumsikia, ameshampigia sana kelele mwanaye aachane naye,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika kwa kuanzia na Aunty Lulu ambapo alikiri kwamba ni kweli ugomvi ulitokea lakini hakuvua nguo.

“Ni kweli tuligombana hapo baa lakini sikuvua nguo na kuhusu kila siku kupigana, jamani hayo ndiyo mapenzi. Wanaosema mimi ndiye namng’ang’ania Amani siyo kweli kwani wote tunapendana,” alisema Aunty Lulu.

Kwa upande wake Amani alifunguka: “Habari hizo siyo za kweli kabisa ndugu mwandishi.”

>>Ijumaa
Aunty Lulu Avua Nguo Hadharani Baada Ya Pombe Kumzidi Kichwa Aunty Lulu Avua Nguo Hadharani Baada Ya Pombe Kumzidi Kichwa Reviewed by BkuHabari Admin on Tuesday, May 13, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.