Unordered List

Definition List

Kim Kardashian Aendeleza Birthday Yake Las Vegas Na Kanye, North West Ajitafutie Kazi Mwenyewe

Its Kim Kardashian birthday!!!
Staa huyu aliyezaliwa katika familia maarufu zaidi ulimwenguni aliweza kutimiza miaka 34 siku ya tarehe 21 October.

Kim katika ujio wa birthday yake aliweza kufanyiwa surprise party na Kanye West sehemu ya Hawaii na sasa wawili hawa wameamua kuextend sherehe hio hadi Las Vegas’ Tao nightclub.

Ok kama umekuwa ukifuatilia miondoko ya Kim Kardashian utagundua kuwa staa huyu ni tamaduni ya kwake kufanya birthday akiwa Las Vegas...na kama kawaida hakuweza kumuacha dadake wa karibu Khloe Kardashian kusherehekea pamoja katika tukio zima akiwa pamoja na marafiki wa karibu wa familia.

Kabla kutua kwa mji huo wa Sin City, Kim pamoja na team yake nzima waliweza kupiga mapicha nje ya private jet yao specially ya tukio hilo.

Cheki baadhi ya mapicha yaliyopigwa na mapaparazi yakimwonyesha Kim pamoja na Khloe, Kanye, na marafiki.



So North West yuko wapi? Kim alifunguka kuwa Nori atajitafutia vya kwake na asitarajie kumtegekea Kim milele kimaisha. Hili ni tukio baada ya Kimye kudaiwa kuwa wanamharibu mtoto wao kifedha.
Kim Kardashian Aendeleza Birthday Yake Las Vegas Na Kanye, North West Ajitafutie Kazi Mwenyewe Kim Kardashian Aendeleza Birthday Yake Las Vegas Na Kanye, North West Ajitafutie Kazi Mwenyewe Reviewed by Admin on Saturday, October 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.