Unordered List

Definition List

Bifu La Diamond Platnumz Na Ali Kiba Kumbe Limeanzishwa Na Wachache Kwa Ajili Ya Biashara


Baada ya kuanzisha mashindano ya mbio kati ya farasi(Diamond) na kobe(Ali Kibaa) na kutaka kuiaminisha dunia kuwa kobe ana mbio kushinda farasi, hatimaye ile miradi iliyotangazwa kwa nderemo na vifijo imeanza miradi hiyo yote inaonekana ilibuniwa kwa ustadi kabisa kwa kumtumia Ali Kiba na mtu aliyepo juu katika game ili kusudi pesa zipatikane kwa watu hao.

Miradi hiyo ni pamoja na Tshirt zilizoandikwa Kiba ni mfalme wa muziki, Diamond mwisho Tandale mjini kote ni Kiba, Cd zilizoandikwa Kiba V Diamond, kwa mtu yeyote mwenye akili atagundua kumbe lile zomeazomea na mambo ya ajabu kama Diamond eti alisema mbeya hamna hoteli ya yeye kulala ilikuwa ni mipango ya watu wachache ya kutengeneza hela, laiti ingekuwa siasa ungesema ni siasa za maji taka,

Kumbe hili bifu la kupikwa lilianzishwa ili watu fulani wapate hela na kwa uhunguzi wangu hawa watu wanajiita Team Kiba. Imani yangu ni kwamba mashabiki wa Kiba wapo tena wastaarabu lakini hizi hype zilizoanzishwa za Kiba V Diamond ni kwa ajili ya manufaa ya watu wachache ambao kwa maslahi yao wanataka kumchafua "Chibu Dangote" ili waje kutuuzia Tshirt na Cd zao uchwara ,kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuvaa Tshirt imeandika Diamond mwisho Tandale!!!
Bifu La Diamond Platnumz Na Ali Kiba Kumbe Limeanzishwa Na Wachache Kwa Ajili Ya Biashara Bifu La Diamond Platnumz Na Ali Kiba Kumbe Limeanzishwa Na Wachache Kwa Ajili Ya Biashara Reviewed by Admin on Friday, October 31, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.