Unordered List

Definition List

Dida Na Ezden Wakutana Coco Beach. Kila Mmoja Ajifanya Hamjui Mwenzie

Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani

WATANGAZAJI wawili waliokuwa wanandoa kabla ya kutengana hivi karibuni, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne, mwishoni mwa wiki walikaushiana kama watu wasiofahamiana baada yakukutana katika hafla iliyofanyika katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Wawili hao walikutana wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo wa Namchukua wa Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambapo mwanaume alikuwa mshereheshaji huku mke akiwa miongoni mwa wageni waalikwa.

Hata hivyo, Dida alionekana kuwa na mbwembwe zaidi huku akipiga ulabu na kuonekana kukolea kiasi cha kujiachia na kukata mauno mbele ya halaiki ya watu pasipo kujali uwepo wa mumewe huyo wa zamani, ambaye alikuwa mpole na aliondoka eneo hilo mara tu baada ya kumalizika kwa shughuli iliyompeleka.
GPL
Dida Na Ezden Wakutana Coco Beach. Kila Mmoja Ajifanya Hamjui Mwenzie Dida Na Ezden Wakutana Coco Beach. Kila Mmoja Ajifanya Hamjui Mwenzie Reviewed by Admin on Wednesday, October 22, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.