Unordered List

Definition List

Wema Kushindwa Kumzawadia Diamond Platnumz Wengi Waliona Ni Lile Pigo La Morano

Na Mayasa Mariwata

STAA wa filamu Bongo, Wema Isaack Sepetu ameshindwa kujibu mapigo ya mwandani wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kutompa zawadi yoyote katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar.

Kutokana na msanii Diamond kumpa zawadi ya gari aina ya Nissan Morano mwandani wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa japo hakuwepo na kumuachia mama yake amkabidhi, mashabiki wengi walikuwa na kiu ya kutaka kujua ni kipi ambacho Wema angemzawadia mpenzi wake katika siku hiyo ili kudhihirisha upendo wake ikiwemo kwa mashabiki kama alivyofanya Diamond.

Mpaka shughuli inaisha watu mbalimbali walijitokeza kutoa zawadi zao huku wengine wakimmwagia noti pamoja na managent yake kumzawadia gari aina ya BMW X6 lakini mwanadada huyo alishindwa kuonyesha makeke yake mpaka mwisho wa shughuli na kubaki akijilaumu; “Hee halafu sijui kwa nini mpaka shughuli imeisha eti sijatoka kumpa zawadi baby wangu, sasa mbona hakuna aliyenikumbusha?”alisema Wema mwisho wa shughuli hiyo.
Wema Kushindwa Kumzawadia Diamond Platnumz Wengi Waliona Ni Lile Pigo La Morano Wema Kushindwa Kumzawadia Diamond Platnumz Wengi Waliona Ni Lile Pigo La Morano Reviewed by Admin on Friday, October 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.