Unordered List

Definition List

Ray C Atia Kidole Swala La Chidi Benz Kunaswa Na Bangi

Ray C ametia kidole swala la Chidi Benz kushikwa na misokoto ya bangi na jeshi la polisi.

Katika akaunti yake ya Instagram Ray C alitoa ushauri naswaha kwa Chidi kuacha mwendeko wake wa kutumia vileo.

Cheki post yenyewe:
"Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako, Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu! nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!! Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika, Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tenakwenye Sanaa,Tumuombee mema.........Tanzania Stand Up n Wish Him Luck............With Love,Ray C Foundation."

Ray C ni mwanzilishi wa Ray C Foundation ambayo nia yake kuu ni kuzindua watu kutotumia madawa ya kulevya.
Ray C Atia Kidole Swala La Chidi Benz Kunaswa Na Bangi Ray C Atia Kidole Swala La Chidi Benz Kunaswa Na Bangi Reviewed by Admin on Saturday, October 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.