Unordered List

Definition List

Jackline Wolper Ampa Makavu Mkongo Anayedai Alikuwa Na Uhusiano Naye

Stori: Erick Evarist


MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper, amemtolea uvimu pedeshee maarufu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu na kumwambia aache kumfuatafuata.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkongo huyo ambaye anajitapa kuwa ameshatembea na baadhi ya mastaa Bongo akiwemo Wolper, alikaririwa katika gazeti hilihili akidai ametembea na Wolper kisha kumwaga na sasa anamwendea mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema anamshangaa mwanaume huyo amekuwa akimfuatafuata na kumzungumzia katika vyombo vya habari wakati hana hadhi ya kuwa na mtu kama yeye “Kwangu mimi huyo mwanaume siyo hadhi yangu, ni mshamba, limbukeni asiyeweza kuniweka mjini…kifupi nimwambie akome kunizungumzia mimi siyo taipu yake, atafute wa saiziyake,” alisema Wolper.

“Nilikutana naye Nairobi aliposema ana shida ya kikazi ndiyo akaanza kuleta mambo ya kunitongoza, nilipomfuatilia nikaona si mtu mzuri, hazimo kidogo. Huwezi kuwa mwanaume ambaye unaropokaropoka hovyo, mimi nina mtu wangu namuheshimu, akome kunizungumzia.”
Jackline Wolper Ampa Makavu Mkongo Anayedai Alikuwa Na Uhusiano Naye Jackline Wolper Ampa Makavu Mkongo Anayedai Alikuwa Na Uhusiano Naye Reviewed by Admin on Saturday, October 11, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.