Unordered List

Definition List

Chris Brown Audhi Mafans Wake Baada Ya Kupost Tweet Kuhusu Ebola

Mwimbaji mashuhuri duniani ,Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake.

''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu duniani...janga hili linatisha kweli,'' aliandika Brown.

Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake na ambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikimye.

Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet. Hata hivyo watu hawakufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana chakusema.

Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi. Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.
Chris Brown Audhi Mafans Wake Baada Ya Kupost Tweet Kuhusu Ebola Chris Brown Audhi Mafans Wake Baada Ya Kupost Tweet Kuhusu Ebola Reviewed by Admin on Wednesday, October 15, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.