Unordered List

Definition List

Polisi Waonya Vikali Baada Ya Chidi Benz Kunaswa Na Bangi


Kufuatia tukio la Msanii wa muziki Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Kupambanana Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aonya vijana kutokujihusha na dawa hizi kabisa.

Kamanda Nzowa amesema kuwa tukio la kukamatwa kwa msanii huyu mkubwa, ni nafasi ya jamii na vijana kujifunza na kuachana na dawa hizi ambazo madhara yake kwa jamii ni makubwa.

Chidi baada ya upekuzi alipatikana na kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi, tukio ambalo limeendeleakuzua maoni tofauti kutoka kwa watu mtandaoni wakati huu ambapo anasubiri hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
Polisi Waonya Vikali Baada Ya Chidi Benz Kunaswa Na Bangi Polisi Waonya Vikali Baada Ya Chidi Benz Kunaswa Na Bangi Reviewed by Admin on Sunday, October 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.