Unordered List

Definition List

Bifu la Waigizaji Kati ya Flora Mvungi na Nisha Lafika Pabaya

Stori: Gladness Mallya

WASANII wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ya hivi karibuni kuwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kupitana kama hawafahamiani.

Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu, Wastara Juma iliyofanyika katika ukumbi wa Dar West uliopo Tabatajijini Dar es Salaam. Wawilihao walikutana mlangoni wakati wa kuingia, lakini Flora alimpita Nisha kama hamfahamu na kama hiyo haitoshi, walipoingia ndani, kila mmoja alikaa meza yake.

Wakati sherehe zikiendelea, ukafika wakatiwa kufungua shampeni na baada ya tukio hilo, Nisha alipewa jukumu la kuwagawia wageni waalikwa kwa kuwamiminia kwenye grasizao, lakini alipofika kwenye meza aliyokaa mwenzake, Flora alikataa glasi yake kuwekwa kinywaji hicho.

Baada ya tukio hilo, paparazi wetu aliwafuata mastaa hao na kuwauliza kulikoni, na Flora alisema: “Sikumuona Nisha mimi, na shampeni nimekataa kwa sababu huwa siipendi.”Kwa upande wake, Nisha alisema: “Mimi sikumuona Flora, kuhusu Shampeni mbona nilimimina kwenye glasi zote jamani!”
Bifu la Waigizaji Kati ya Flora Mvungi na Nisha Lafika Pabaya Bifu la Waigizaji Kati ya Flora Mvungi na Nisha Lafika Pabaya Reviewed by Admin on Wednesday, October 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.