Unordered List

Definition List

Alichofanyiwa Diamond Platnumz #SerengetiFiesta Si Mpango Kabisaa

Nakumbuka miaka mitano iliyopita aliyekuwa nguli wa filamu Nchini Tanzania marehemu ""Steven Kanumba"" alienda kwenye jumba la Big Brother....

Amini usiamini bila sababu yeyote ya maana watanzania ndo walikuwa wa kwanza kuanza kumsema kuwa hajui kuvaa, nani alimchagua , hajui kiingereza mpaka kufikia kumuigiza!!!

Walisahau hata watu maruufu kama Messi na wengine wengi hawajui kuongea kabisa lugha hiyo..

Baada ya kifo chake watanzania hawa hawa wakaanza kusema alikuwa nguli aliyetuwakilisha vizuri nje ya nchi na kulia sana!!! kumbe wakati akiwa hai tulikuwa tunamshusha chini..

Miaka mitano baadae Tanzania imempata mtu anayeiwakilisha vizuri nje ya mipaka na kuitangaza vizuri nchi yake..

Pasipokuwa na sababu za msingi (chuki binafsi tu) anapangiwa njama za kuzomewa na kuabishwa katika ardhi ya nchi yake ambayo kwa namna moja au nyingine kuna watu wameifahamu sababu yake!!

Ukiuliza sababu za wengi wao kumchukia ni mafanikio yake lakini hatakama humpendi mtu hivi ndo hadi umzomee kwa kiasi kile !!!

Leo na kesho naye huyu akitoka utaskia hawa hawa waliokuwa wanamzomea wanaanza kusema jamaa alikuwa anatuwakilisha vizuri sana , ametutangaza sana kimataifa!! lakini Watanzania wenzake ndio vinara wa kumuangusha..

Si lazima kila mtu ampende Diamond ila kutumia nguvu kubwa sana kumuangusha mtu niishara ya uwoga na Roho ya kimaskini...

Nimeamini ""maisha bila unafki hayaendi"
Alichofanyiwa Diamond Platnumz #SerengetiFiesta Si Mpango Kabisaa Alichofanyiwa Diamond Platnumz #SerengetiFiesta Si Mpango Kabisaa Reviewed by Admin on Sunday, October 19, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.