Unordered List

Definition List

Lady Jey Dee Anauhusiano Wa Kimapenzi Na AY?

Stori: Andrew Carlos

KABANG! Mwanadada asiyechuja kwenye muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ mwishoni mwa wiki iliyopita alibambwa ‘laivu’ kwa mara ya kwanza katika kipindi kirefu akiwa ‘very close’ na mwanamuziki mwenzake, Ambwene Yessaya ‘AY’ wakiteta jambo.

Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa High Spirit uliopo Jengo la IT Plaza, Posta jijini Dar ambapo kulikuwa na uzinduzi wa huduma mpya ya mtandao wa Airtel huku mastaa mbalimbali na waandishi wa habari wakijumuika pamoja kuanzia saa 1:00 usiku.

Mapema kabla ya uzinduzi huo, AY aliyekuwa amepiga pamba nyeusi alikuwa wa kwanza kutinga ukumbini hapo akiwa ameongozana na Mtangazaji wa Show ya Mkasi kupitia EATV, Salama Jabir.

Wakiwa wanapiga stori za hapa na pale, mara Jide naye alitinga ukumbini hapo ambapo jicho lake lilitua kwa AY na kusogea karibu kwenda kusalimiana naye.

Wakiwa katika maongezi Jide na AY, mshereheshaji aliyekuwa akiendesha uzinduzi huo, Ephraim Kibonde aliwataka wakae mbele ikiwa ni kusaidia kuendesha shughuli ya ufunguzi wa huduma hiyo kama majaji.Katika uzinduzi huo, waandishi na wahudhuriaji walikuwa wakishindana kuimba na kupewa zawadi kama head phones, simu aina ya Samsung Galaxy III pamoja na spika ndogo kutoka kampuni kubwa ya kutengeneza bidhaa za muziki iitwayo Beats.

Jide alionekana kukubali wito huo wa kukaa na AY ambapo aliamua kuwatema wenzake aliokuwa ameongozana nao hapo ukumbini na kwenda kukaa mbele na AY, vivyo hivyo kwa AY naye aliwatema akina Salama na mshikaji wake na kwenda mbeleKatika hali nyingine ya kuduwaza, Jide akiwa na AY huku wakionekana wako ‘dipu’ kwa mazungumzo kabla ya kuanza kuwajaji waimbaji, alionekana kukolea na kinywaji alichokuwa anakunywa bila kutumia glasi (kupiga tarumbeta) mwanzo mwisho.

Mara kwa mara wawili haowalikuwa bize wakiteta kwa sauti ya chini kwa takribani nusu saa.
GPL
Lady Jey Dee Anauhusiano Wa Kimapenzi Na AY? Lady Jey Dee Anauhusiano Wa Kimapenzi Na AY? Reviewed by Admin on Friday, October 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.