Unordered List

Definition List

Diamond Platnumz Atajwa Msanii Wa Mwezi Oktoba (#AoTM) Na MTV Base

Kando na kushiriki katika tuzo za MTV MAMA miezi kadhaa iliyopita, Diamond Platnumz sasa mwezi huu wa Oktoba amechaguliwa kama msanii wa mwezi katika channel ya MTV Base.

Hii ni kuashiria kuwa Diamond Platnumz atafanyiwa kampeni ya hali ya juu huku maisha yake ya usanii yakiangaziwa kwa undani katika channel hio.

Kampeni hii inayojulikana kama (#AoTM) itamuangazia maisha ya Diamond na mambo aliyopitia katika kurekodi video zake pamoja na tours ambazo amefanya.

Hivi majuzi nchini Afrika Kusini, MTV Base ilikuwa ikifanya video shootings na Diamond ili kufanikisha kampeni nzima ya staa huyu ambaye sahizi anawika na kibao 'mdogo mdogo'

Mwezi jana msanij wa mwezi alikuwa ni Casper Nyovest wa Afrika Kusini.
Diamond Platnumz Atajwa Msanii Wa Mwezi Oktoba (#AoTM) Na MTV Base Diamond Platnumz Atajwa Msanii Wa Mwezi Oktoba (#AoTM) Na MTV Base Reviewed by Admin on Thursday, October 02, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.