Unordered List

Definition List

Justin Bieber Ampiga Paparazi Ngumi Jijini Paris

Justin Bieber muda huu yuko jijini Paris, Ufaransa  katika harakati za fashion week ambazo ziliendelea kufanyika wiki iliopita. Bieber ameonekana akitangamana na Kardashian family ikiwemo model Kendall Jenner, Kim Kardashian, Paris Hilton na Selena Gomez.

Katika tukio lililofanyika siku ya jumanne, kulingana na TMZ linadai kuwa limenasa picha za Justin Bieber akivurugana na mapaparazi ambao walikuwa wakimuandama kama upepo.

Kulingana na picha zimemuonyesha Bieber akimsukuma mmoja wa mapaparazi na nyingine ikimuonyesha akimrushia ngumi paparazi aliyekuwa ameshikilia kamera.
Picha zikimuonyesha Bieber katika harakati za kuwadhalilisha mapaparazi
Akiwa amevalia gwanda la kijeshi na viatu vyeusi, imeonyesha dalili kuwa Justin Bieber hataki machezo
Carine Roitfeld party ambapo Beiber alitangamana na Kardashians na wengine

Justin Bieber Ampiga Paparazi Ngumi Jijini Paris Justin Bieber Ampiga Paparazi Ngumi Jijini Paris Reviewed by Admin on Wednesday, October 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.