Unordered List

Definition List

Wiz Khalifa Aanikwa. Picha Za Mapacha Aliokuwa Akichepuka Nao Zawekwa Mtandaoni

Siku ya jana (Jumatano) iliwekwa wazi kuwa Wiz Khalifa alikuwa akimwendea kinyume kimapenzi Amber Rose na madada ambao ni mapacha, well picha zao zimeanikwa kwa mtandao

Jas and Ness Rose (hana uhusiano wowote na Amber) ni fashion designers na madada maarufu katika tasnia ya hip hop na mara kadhaa washawahi kuonekana na mastaa kama Kanye West na pia Chris Brown.

Mapacha hawa wakati flani mwezi Juni waliweza kupiga picha Instagram wakiwa na Wiz Khalifa lakini picha hizo zimeonekana zimefutwa.

Baada ya Amber Rose kufunguka kwa Twitter kuwa Wiz Khalifa anamwendea kinyume kimapenzi, Amber aliwaambia marafiki zake kuwa alikuwa akimshuku Wiz Khalifa kwa muda mrefu lakini alikuwa anatafuta ithibati thabiti.

Amber Rose wiki jana alitia sahihi za kumpata talaka Wiz Khalifa.
Wiz Khalifa Aanikwa. Picha Za Mapacha Aliokuwa Akichepuka Nao Zawekwa Mtandaoni Wiz Khalifa Aanikwa. Picha Za Mapacha Aliokuwa Akichepuka Nao Zawekwa Mtandaoni Reviewed by Admin on Thursday, October 02, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.