Unordered List

Definition List

Ney Wa Mitego Afunguka Kuhusu Ishu Ya Kuwarushia Maji Mashabiki; Si Ushirikina

Kama utakuwa unafuatilia show za Nay wa Mitego, utakuwa umeshuhudia akiwamwagia maji mashabiki wake chupa mbili mpaka tatu. Kitendo hicho kimewafanya baadhi ya watu wahoji lengola ‘stunt’ hiyo.

Nay ameiambia Bongo5 kuwa kufanya hivyo ni kuwatia mzuka mashabiki wake na sio kama wengine wanavyotafsiri kuwa ni agizo la mganga.

Rapper huyo amesema katika maisha yake hajawahi kwenda kwa mganga. “Nilijua watu wataanza kuzungumza kuhusu yale maji ambayo nayatumia. Kitu ambacho ninaweza nikasema yale ni maji ya kawaida, sijui ni nini kimenijia kichwani, nikaamua nitumie maji na ninashangaa tu huwa nikitumia maji kuwamwagia watu wanakuwa kama wanapagawa hivi! Mzuka unakuwa juu zaidi yaani sijui ni kwanini inakuwa hivyo. Nimesikia hilo suala, sifanyi hivyo ili kutimiza agizo la mganga na maji ambayo huwaga nayatumia ni yale ambayo tunawekewaga kwa ajili ya kunywa.

Sijawahi kwenda kwa mganga wala sina chale niliyochanjwa ili muziki lwangu u-shine,” amesema Nay.
Ney Wa Mitego Afunguka Kuhusu Ishu Ya Kuwarushia Maji Mashabiki; Si Ushirikina Ney Wa Mitego Afunguka Kuhusu Ishu Ya Kuwarushia Maji Mashabiki; Si Ushirikina Reviewed by Admin on Friday, October 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.