Unordered List

Definition List

Kim Kardashian Amwaga Mtama Kuhusu Ndoa Yake Na Kanye West

Kim Kardashian ameamua kuwa anataka harusi yake iwe ndogo, na hadhira kubwa zaidi.

Staa huyu wa Keeping Up With The Kardashian jana alikuwa akihojiwa na Ryan Seacrest katika radio ya  KIIS FM na alitoa fununu kuhusu harusi yake na Kanye West.

Mpaka kufikia sasa uvumi unasema kuwa harusi ya wawili hawa itafanyika mwezi Mei na itakuwa jijini Paris.

'Tutakuwa na harusi ndogo sana na yenye mapenzi" Kim aliongea kwa kumwambia producer wa kipindi hicho. "Pindi muda mnavyosongea tumegundua kuwa tunahitaji kuwa na watu kidogo katika harusi yetu na pia kuifanya ya kimapenzi kuliko vile watu wanavyofikiria"

Kim hakutoa fununu zozote kuhusu lini ama wapi harusi yao itakapofanyika na alionekana kuwa mtu asiyekuwa na haraka yeyote.

"Napenda maisha ninayoishi kwa sasa, na mtoto wangu North West ni kipenzi changu kuliko chochote...na napenda kuwa mzazi" Kim alizidi kufunguka kuhusu maisha yake.


Kim Kardashian Amwaga Mtama Kuhusu Ndoa Yake Na Kanye West Kim Kardashian Amwaga Mtama Kuhusu Ndoa Yake Na Kanye West Reviewed by Admin on Wednesday, February 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.