Unordered List

Definition List

Je Wawajua Wote Waliomfikisha Snura Pale Alipo Sasa?!?

snura wema
Wakati narekodi wimbo wangu wa kwanza Wema Sepetualihusika sana…hela yake ilihusika studio, sauti yake ilihusika kwenye wimbo huo ambao ni shogaake mama …vazi langu la show kwa mara ya kwanza wema ndio alinibunia na mimi nimeliandeleza vazi hilo mpaka leo kwenye show zangu sina chakukulipa wema ila nakushukuru sana nakuombea kwa mungu akubariki zaidi na zaidi wema sepetu…Ningependa kuanza na movie kabla ya muziki…japokua mwaka huu nimefanya vizuri sana katika muziki…basi kama kuna mtayarishaji wa movie anae tambua na kuthamini kipaji changu ni chekibudi ….nakushukuru sana kakaangu chekbud kwa kutambua umuhim wangu asante sana kaka ….nadhani kama ww nimshabiki wangu kwenye movie utakubaliana na hilo hakuna movie ya chekibudi mimi sipo…nakutakia kila lakheri brother. ….shukrani zinaendelea fuatilia ujue nani anafuata wako wengu kuna vitu vingi sana mtavijua ambavyo naamini hamjawahi kuvisikia mtavijua kupitia mtiririko huu wa shukrani…..
snura dude

Tundaman ndio mtu alie tumia nguvu kuniingiza kwenye muziki baada ya kuona kama siwaelewi hivi kila waliponiambia ….wakati anazindua albamu yake ya Starehe Gharama pale Maisha aliamua kutengeneza tangazo ambalo lilisema Snura atatambulisha wimbo wake mpya kwa mara ya kwanza kiukweli alinivuruga kwa sababu mimi sikua na wimbo wowote sasa kwa kuhofia aibu nishatangazwa ndio nikalazimika kwenda kurekodi shogaake mama haraka sana na nikafanya hiyo show watu wakanielewa sana huo ndio ulikua mwanzo ….leo hii nimeona faida yake asante sana kakaangu tunda man mungu akubariki sana umekua mtu muhim sana kwenye maisha yangu tuendelee kushikana hivihivi….

snura tunda man
Marehemu Sharo Milionea alinipigia kelele sana nifanye muziki yalikua yanaingilia huku na kutokea kule…..najua utakua una jiuliaza kwann nimemuweka wakati alishafariki …nimefanya hivi kwasababu ktk miaka yote mwaka 2013 ndio umekua wa mafanikio sana kwangu na sababu ni mziki ambao huyu ndio mtu aliekua akinipigia kelele sana nifanye sijui kwann sikumsikilizaga natamani angekuepo aone kile alichokua anakitamani aone watanzania na nje ya tanzania walivyonipokea vizuri…
snura sharo millionea
Je Wawajua Wote Waliomfikisha Snura Pale Alipo Sasa?!? Je Wawajua Wote Waliomfikisha Snura Pale Alipo Sasa?!? Reviewed by Admin on Monday, February 03, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.