Unordered List

Definition List

Aunt Ezekiel Azidiwa Na Presha, Alazwa Hospitali

STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuanguka ghafla kwa presha akiwa ‘location’ jijini Tanga, Risasi Jumamosi lina habari hii.

Kwa mujibu wa chanzo, Aunt  akiwa katika harakati za kuigiza filamu anayocheza na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, ghafla alianguka na kukimbizwa katika Hospitali ya Gesha jijini humo.

Baada ya kuzipata habari hizi, mapaparazi wetu walimtafuta Aunt kwa njia ya simu  na alipopatikana alikiri kuanguka kutokana na kusumbuliwa na presha ya kushuka.


 “Kweli  nilikuwa shutting na Mzee Majuto, ghafla nilianguka na kukimbizwa hospitali, wameniwekea dripu mkononi ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri,” alisema Aunt.
Aunt Ezekiel Azidiwa Na Presha, Alazwa Hospitali Aunt Ezekiel Azidiwa Na Presha, Alazwa Hospitali Reviewed by Admin on Saturday, February 22, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.