Unordered List

Herieth Chumila: Bongo Movies Imeniroga

Definition List

Unaamini kurogwa? Hebu msikie huyu! Baada ya kuugua kwa muda mrefu, msanii wa filamu za Kibongo ambaye alikuwa ni mama mlezi wa klabu ya waigizaji ya Bongo Movie Unity (Bongo Muvi), Herieth Chumila, amefunguka kuwa ametupiwa majini na wenzake katika tasnia hiyo.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Herieth alisema ni muda mrefu tangu alipoanza kuugua ambapo alikwenda hospitali mbalimbali, kwa mashehe na kutumia dawa za kienyeji zikiwemo za โ€˜ki-sunnaโ€™ lakini hakukuwa na mafanikio yoyote kwani hakugundulika kuwa na ugonjwa wowote.

Alisema kila alipokuwa akiombewa, majini yalikuwa yanasema yametokea Bongo Movie Unity na sababu za kutupiwa ni kwa kuwa eti alijiingiza kwenye kila kitu hivyo wakaamua kumkomesha. Baada ya kushindikana kote huko, Herieth kwa sasa anashinda kanisani kwa Nabii Yasip Bendera wa Kanisa la Ufunuo huko Yombo-Buza, Dar, akiombewa na afya yake inaendelea vema.

โ€œKweli uchawi upo, hao Bongo Movie wamenitupia majini. Jamani nimeugua sana ila kwa sasa ninaendelea vizuri baada ya kuombewa. Namshuru sana Mungu kwa kunipa nafuu,โ€ alisema Herieth kwa uchungu. Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere hakupatikana kwa simu kujibu madai hayo..
Herieth Chumila: Bongo Movies Imeniroga Herieth Chumila: Bongo Movies Imeniroga Reviewed by Admin on Thursday, February 06, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.