Unordered List

Definition List

Snura Amrushia Maneno Shilole. Cheki Alichokisema Hapa

MAMA wa majanga, Snura Antony Mushi kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumzia kauli ya  msanii mwenzake wa muziki wa mduara, Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole’ juu yake kuwa ameisha kimuziki ndiyo maana ameamua kukimbilia muziki wa Taarab.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Snura ambaye anawika mitaani kwa ngoma kali kama Majanga na Nimevurugwa, alisema kitendo cha Shilole ‘kuponyokwa’ na maneno hayo ni ishara tosha kuwa anamkubali na kufuatilia kazi zake kwa ukaribu mkubwa.

Snura
“Sina tatizo na maneno ya Shilole, hiyo ni ishara kuwa anafuatilia na kuzikubali sana kazi zangu, wala hawezi kunizuia kufanya kazi zangu kwa namna ambavyo nafikiria, yeye afanye yake, nami nishike ‘hamsini zangu’, alisema Snura.
Snura Amrushia Maneno Shilole. Cheki Alichokisema Hapa Snura Amrushia Maneno Shilole. Cheki Alichokisema Hapa Reviewed by Admin on Thursday, February 20, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.