Unordered List

Definition List

AT Na Kashfa La Kutumia Nguvu Za Kiza Kufaulu Kimziki Zaanikwa!!

Mganga kwa jina Shariffa na anayedai kuwa amemfanikisha msanii AT kufaulu kimziki sasa amejitokeza live kwa wananchi kudai kuwa anamdai staa huyu anayevuma kwa nyimbo zake kuwa anamdai deni la laki tisa.

Kulingana na mganga huyu anadai kuwa AT kawaida humtembea kabla hajatoa nyimbo zake.
‘‘Tangu bado hajafahamika yaani sio mwanamuziki mimi nilikutana naye Zanzibar Unguja, tena nakumbuka kwa mara ya mwisho alikuja na Gerry Rhymes lakini Gerry alikuwa afahamu kitu chochote, chakushangaza tangu nilipomfanikishia mahitaji yake maana mimi ni mganga basi amenisahau kabisa nikijaribu kumpigia simu hapokei mpaka anapokei tuzo anapata safari za kwenda muscat amenisahau mimi ninaomba anipatie vile vitu alivyoahidi kwangu anipatie,sio kwa ugomvi ila sheria zetu sisi waganga kwasababu hizi ni kazi namdai deni la laki tisa nikimpigia simu hapokei ndio maana nimekuja hapa kuripoti’Alisema Mganga huyo.

AT alipojaribiwa kuulizwa kuhusu kama ana uhusiano wowote na mganga huyu AT alikana na kudai kuwa kuna watu wamejitokeza kumharibia jina na wengine kujitafutia umaarufu wenyewe.
AT Na Kashfa La Kutumia Nguvu Za Kiza Kufaulu Kimziki Zaanikwa!! AT Na Kashfa La Kutumia Nguvu Za Kiza Kufaulu Kimziki Zaanikwa!! Reviewed by Admin on Tuesday, February 04, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.