Unordered List

Definition List

Whatsapp Imenunuliwa Na Facebook!!!!

Imekuwa rasmi!! Mtandao wa kutuma meseji fupi wa Whatsapp umenunuliwa rasmi na mtandao wa Facebook.

Mtandao huu umenunuliwa na Facebook kwa gharama ya $19 bilioni.

Mtandao huu utalipwa kwa mtindo, $ 4 bilioni utalipwa kupitia pesa mkononi, $12 bilioni kupitia uwekezaji wa soko na $ 3 bilioni kwa uwekeza mwingine.



Makubaliano haya yameifanya Facebook kuwa mtandao wa nguvu zaidi haswa baada ya utafiti kuonyesha kuwa wengi wanahamia Whatsapp kutoka Facebook.

"Hakuna mtu ashawahi kufanya jambo kama hili katika historia ya binadamu" Mark Zuckerberg aliwaambia wanahabari kuhusu Whatsapp. Mtandao huu umeweza kupata watumiaji 450 milioni kwa muda wa miaka mitano.

Whatsapp ni mtandao ulioanzishwa na mzaliwa wa Ukraine Jan Khoum,ambaye aliacha masomo katika college na kuhamia nchini Marekani kama mhamiaji haramu.

Zuckerberg ambaye pia aliununua mtandao wa Instagram aliweza kutoa maoni ya kununua mtandao huo siku kumi zilizopita wakati walipokuwa wakijivinjari mankuli ya jioni.

Haijajulikana Facebook wana haja au wataitumia Whatsapp kwa njia gani lakini tujuavyo sisi ni kuwa jamaa kuacha masomo halafu kupewa bilioni 19 dola za kimarekani ni  mshangao mkuu.

Waonaje pia wewe uache masomo?
Whatsapp Imenunuliwa Na Facebook!!!! Whatsapp Imenunuliwa Na Facebook!!!! Reviewed by Admin on Thursday, February 20, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.